UTABIRI WA HALI YA H...
UTABIRI WA HALI YA HEWA KATIKA BONDE LA PANGANI MWEZI MACHI 2026
11 Mar, 2026
UTABIRI WA HALI YA HEWA KATIKA BONDE LA PANGANI  MWEZI  MACHI 2026

TAARIFA YA UTABIRI WA HALI YA MVUA MWEZI FEBRUARI, 2026- BONDE LA PANGANI
WIKI YA KWANZA

Katika Vidakio vya Bonde la Pangani kunatarajiwa kuwa na hali ya mvua kwa maeneo mengi huku ikitabiriwa hali ya mvua kubwa yenye wastani wa zaidi ya Milimita 200 katika Kidakio cha Zigi ikijumuisha maeneo ya Wilaya ya Mkinga na Muheza. Kidakio cha Kikuletwa maeneo ya Mkoa wa Arusha na Kilimanjaro kutakuwa na mvua ya wastani wa kati ya milimita 1 hadi10. Halikadhalika maeneo ya Kidakio cha Mkomazi, Luengera,Pangani main na Msangazi yanatarajiwa kuwa na mvua zenye wastani wa kati ya Milimita 20 hadi 200 kwa maeneo mengi ambayo hujumuisha Wilaya ya Simanjiro, Same, Handeni, Muheza na Pangani.
• WIKI YA PILI

Kidakio cha Pangani main ikihusisha (Wilaya ya Mwanga, Simanjiro,Same na Korogwe),Vidakio vya Ruvu,Mkomazi,Umba na Luengera kwa pamoja kukitarajiwa kuwa na mvua kiasi ya wastani kati ya Milimita 20 na 100 kwa maeneo mengi. Halikadhalika maeneo yaliyosalia katika Vidakio vya Zigi na Msangazi vinatarajiwa kuwa na mvua kiasi kwa wastani wa chini ya Milimita 20 ikijumuisha maeneo ya wilaya ya Handeni na Pangani.

• WIKI YA TATU

 Vidakio vya Bonde la Pangani kunatarajiwa kuwa na hali ya mvua zenye wastani wa Milimita 10-200 kwa mengi ya Vidakio ikijumuisha Kidakio cha Kikuletwa (Mkoa wa Arusha na Kilimanjaro), Pangani main (Wilaya za Korogwe na Simanjiro), Msangazi wilaya ya Handeni. Halikadhalika baadhi ya maeneo ya Kidakio cha Luengera Wilaya ya Korogwe na Msangazi Wilaya za Handeni na Pangani main Wilaya ya Simanjiro yanatarajiwa kuwa na mvua za wastani wa Milimita 20-100 kwa maeneo mengi.
• WIKI YA NNE

Kidakio vilivyopo ndani ya Bonde la Pangani kuna matarajio ya kuwa na hali ya mvua kwa wastani wa milimita 5-20 kwa upande wa Kidakio cha Pangani main ikijumuisha maeneo ya Wilaya za Simanjiro na Same pamoja na Kidakio cha Mkomazi, Umba katika Wilaya ya Lushoto. Halikadhalika maeneo mengine ya Vidakio yaliyosalia haswa Kidakio cha Kikuletwa maeneo ya Mkoa wa Arusha na Manyara na pia Kidakio cha Msangazi ikujumisha maeneo ya Wilaya za Handeni na Pangani yanatarajiwa kuwa na mvua za wastani wa kati ya Milimita