Majukwaa ya Wadau

Bodi imeimarisha mfumo huu shirikishi kwa kuongeza fursa muhimu ya kujadiliana kwa pamoja, kubadilishana uzoefu na kuweka mikakati ya pamoja kupitia uanzishwaji wa majukwaa ya wadau ambapo mpaka sasa Bodi imefanikiwa kuunda Jukwaa la Wadau wa Bonde la Pangani pamoja na majukwaa manne (4) ya vidakio vya Themi, Zigi, Umba na Kikuletwa. Uanzishwaji wa majukwaa haya umeiwezesha Bodi kutambua fursa zilizopo ikiwemo kuweka mipango ya pamoja katika uhifadhi wa vyanzo. Hatua hii muhimu ya ushirikishwaji wa wadau kupitia uundwaji wa majukwaa imeongeza kasi ya kutimiza lengo mahsusi la kuhakikisha kuwa vyanzo vya maji vinatunzwa ili kuongeza upatikanaji endelevu wa Maji katika Bonde la Pangani.

Faida za Majukwaa ya Wadau

  1. Hutoa fursa ya utambuzi wa changamoto za pamoja za usimamizi wa Rasilimali za Maji.
  2. Hutoa fursa ya kubadilishana uzoefu wa kuhusu masuala mbalimbali yahusuyo Rasilimali za Maji miongoni mwa wadau.
  3. Huwezesha kuandaa Mpango wa Pamoja utakaofanikisha utatuzi wa changamoto za Rasilimali za Maji.
  4. Hutumika kama nyenzo muhimu ya kufanikisha Usimamizi Endelevu wa Rasilimali za Maji.

Na

JINA LA JUKWAA

ENEO

1

Jukwaa Kuu la Wadau wa Bonde la Pangani

Bonde la Pangani

2

Jukwaa dogo la Kidakio cha Mto Themi

Eneo bonde la mto Themi

3

Jukwaa la Kidakio cha Kikuletwa

Eneo bonde la Kikuletwa

4

Jukwaa la Kidakio cha Mto Zigi

Eneo bonde la Mto Zigi

5

Jukwaa la Kidakio cha Mto Umba

Eneo bonde la Mto Umba