UTABIRI WA HALI YA M...
UTABIRI WA HALI YA MVUA KATIKA BONDE LA PANGANI MWEZI MEI 2026.
06 May, 2026
UTABIRI WA HALI YA MVUA KATIKA BONDE LA PANGANI MWEZI MEI 2026.

TAARIFA YA UFAFANUZI WA UTABIRI WA HALI YA MVUA KWA MWEZI MEI KWA MWAKA 2026 KATIKA MAENEO YA BONDE LA PANGANI

•    WIKI YA KWANZA  
Katika wiki hii, Bonde la Pangani kunatarajiwa kuwa na hali ya mvua kwa maeneo mengi ya vidakio. Huku utabiri ukionyesha hali ya uwepo wa mvua za wastani wa kati ya Milimita 20–100 kwa kidakio cha Msangazi, Luengela na Kikuletwa (Wilaya za Simanjiro, Handeni, Same na Arumeru. Katika sehemu kubwa ya vidakio vya Pangani main, Ruvu, Mkomazi na Umba imetabiriwa kuwa na hali ya mvua za wastani wa kati ya Milimita 1-20 ikijumuisha sehemu za Wilaya za Mwanga, Same, Mkinga, Simanjiro na Lushoto. 
•    WIKI YA PILI  
Kwa wiki hi,i katika vidakio vya Pangani main, Msangazi, Umba na Ruvu kunatarajiwa kuwa na mvua zenye wastani wa milimita 1-20 kwa maeneo mengi ikijumuisha Wilaya ya Simanjiro, Same, Handeni, Mwanga, Korogwe, Pangani na Lushoto. Hata hivyo, Vidakio vya Luengera na Mkomazi inatabiriwa kuwa na mvua za wastani wa kati ya Milimita 20-50 ikijumuisha maeneo ya Wilaya za Muheza na Mkinga. Hali ya uwepo wa mvua kubwa kwa maeneo machache ambayo yameweza kuonekana katika kidakio cha Kikuletwa na Ruvu kwa wastani wa juu wa kati ya Milimita 50-300 ikijumuisha maeneo ya Wilaya za Siha na Moshi.
•    WIKI YA TATU 
Kwa wiki hii, maeneo mengi ya Vidakio vya Kikuletwa, Mkomazi na Ruvu kunatarajiwa kuwa na mvua zenye wastani wa Milimita 20-300 kwa maeneo mengi ikijumuisha Wilaya ya Arumeru, Siha, Moshi, Rombo, Same na Mwanga. Hali kadhalika, Vidakio vilivyosalia ikiwemo Umba na Pangani main maeneo mengi ya Wilaya za Mkinga, Korogwe na Handeni  zikitarajiwa kuwa na mvua zenye wastani wa kati ya Milimita 1–20 huku maeneo yaliyosalia ya Kidakio cha Msangazi yakionekana kuwa makavu kiasi haswa katika wilaya ya Pangani.
•    WIKI YA NNE
Maeneo mengi ya Bonde la Pangani yametabiriwa kuwa makavu na mvua nyepesi zenye wastani wa Milimita 0-10 kwa maeneo machache kwa ujumla ikijumuisha vidakio vyote vilivyopo. Halikadhalika, katika Kidakio cha Kikuletwa na Ruvu kumetabiriwa kuwa na mvua za wastani wa Milimita 20-100 kwa maeneo yanayozunguka mlima Kilimanjaro.