Vibali vya Matumizi ya Maji

Kibali cha Matumizi ya Maji ni kibali kinachotolewa kisheria kwa mtu/taasisi kwa ajili ya matumizi ya maji kama kunyeshea mashamba, kunywa, viwanda vya maji , mifugo.

Sheria ya usimamizi ya rasilimali za maji ya mwaka elfu mbili na tisa (2009) namba 11, inamtaka kila anayechepusha maji kwenye chanzo chochote cha maji (kisima kirefu, chemchem, mito, mabwawa, maeneo oevu) kwa kutumia miundombinu lazima awe na kibali cha matumizi ya maji kama taratibu zinavyooleza.

Hivyo basi kwa mujibu wa sheria hii, kila anayetaka kutumia maji kwa matumizi yaliyotajwa hapo juu, inabidi awe kibali. Ili kupata kibali cha matumizi ya maji inapaswa afuate taratibu za kuomba kibali kwa matumizi yake ya maji kwa kujaza fomu ya maombi ya kibali cha matumizi ya maji.

Kuomba Kibali cha Matumizi ya Maji Tafadhali Bonyeza Hapa