Kibali cha Uchimbaji

Kwa mujibu wa Sheria Na. 11 ya Usimamizi wa Rasilimali za Maji ya mwaka 2009, Bodi ya Maji Bonde la Pangani ndiyo taasisi inayohusika na kutoa vibali vya uchimbaji wa visima vyenye urefu zaidi ya mita 15 katika Mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Tanga na Manyara (Wilaya ya Simanjiro).

Taratibu za kufuata ili kupata kibali cha kuchimba kisima:

  1. Kabla ya mteja kuomba kibali cha kuchimba kisima anapaswa awe amefanya utafiti wa maji chini ya ardhi kutoka Bodi ya Maji Bonde la Pangani, Taasisi au Kampuni iliyosajiliwa kufanya shughuli za utafiti wa maji chini ya ardhi na Wizara ya Maji.
  2. Mteja anatakiwa kuandika barua ya maombi kwa Bonde pamoja na kujaza fomu “C” ya maombi, ikiwa imeambatanishwa na taarifa ya utafiti iliyofanywa na Ofisi ya Bonde au Kampuni iliyosajiliwa na Wizara ya Maji. Gharama za maombi ya kibali cha kuchimba kisima ni shilingi laki moja na nusu tu (150,000/=) na malipo yatafanyika kwa njia ya kielektroniki baada ya kupewa namba za malipo(control number).
  3. Baada ya kupata kibali cha uchimbaji mteja anaruhusiwa kuanza uchimbaji wa kisima chini ya usimamizi wa Bodi ya Maji au mtaalamu anayetambulika na Wizara(mhaidrojiolojia/fundi sanifu haidrojiolojia).
  4. Kibali cha uchimbaji kinadumu kwa muda wa miezi mitatu tu endapo mteja atashindwa kuchimba kwa muda aliopewa anapaswa kuhuisha kibali chake.
  5. Baada ya kumaliza kuchimba kisima mteja anapaswa kuomba kibali cha matumizi ya maji kabla ya kuanza kuyatumia.