Mkutano Mkuu wa Jumu...
Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Watumia Maji Mto Kihuhwi (JUWAMAKIHU)
28 Jan, 2026 07:30-16:30 PM Tate Plus Hall- Muheza District-Tanga Region
Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Watumia Maji Mto Kihuhwi (JUWAMAKIHU)

MKUTANO MKUU NA UCHAGUZI WA VIONGOZI WA JUMUIYA YA WATUMIA MAJI MTO KIHUHWI -WILAYA MUHEZA

Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Watumia Maji Mto Kihuhwi (JUWAMAKIHU)ulifanyika tarehe 20.1.2026  katika Ukumbi wa Tate Plus Wilaya Muheza na kufunguliwa na Mkuu wa Wilaya Muheza, Mhe. Ayubu Sebabili.

Mkutano huo uliratibiwa na Bodi ya Maji Bonde la Pangani kwa kushirikiana na Wadau wa Maendeleo kutoka Shirika la Kijerumani-GIZ kupitia Mradi wa PROWAS-SASA For green Cities ya Jiji la Tanga.  Mkutano uliwahusisha Wadau mbalimbali wa Mto Kihuhwi katika Kidakio cha Zigi kutoka katika vijiji 16 viliyopo kandokando mwa vyanzo vya Maji vya Mto Kihuhwi-Wilaya ya Muheza, Maafisa Tarafa 2, Waheshimiwa Madiwani  na Watendaji wa Kata 7, Wenyeviti na Watendaji  wa Vijiji-32, Watumia Maji wakubwa na Wadogo pamoja na Wadau wa Uhifadhi wa Mazingira (UWAMAKIZI).

Lengo la Mkutano huo ulikuwa ni kupitia katika ya Jumuiya na kufanya uchaguzi wa kuwapata viongozi wa Kamati  Tendaji wa Jumuiya yenye Wajumbe 6 kwa nafasi za Mwenyekiti,  Makamu Mwenyekiti,  Katibu, Mhazini  na Wajumbe 2 watakaodumu madarakani kwa vipindi vya miaka 3 wakiwa na majukumu muhimu ya kusimamia matumizi endelevu ya rasilimali za maji katika eneo la Mto Kihuhwi na kuwaunganisha wadau wote katika kutunza, kulinda na kugawa rasilimali za maji kwa makundi yote.

Mhe.Mkuu wa Wilaya aliadi kutoa ushirikiano kwa viongozi wa Jumuiya na kuwataka kufanya kazi zao kwa ushirikiano na viongozi wa Serikali na wanasiasa katika eneo la Jumuiya. Vilevile aliwataka viongozi wa VIjiji, Kata na Tarafa kutoa ushirikiano kwa Jumuiya hasa katika kukabiliana na changamoto ya uchimbaji haramu wa madini kwenye vyanzo vya maji . Aliahidi kupitia Kamati ya Usalama wa Wilaya kufanya operesheni maalumu kwa kushirikiana na Bonde la Pangani,  TANGA UWSSA, Ofisi ya Madini, Halmashauri ya Wilaya Muheza na TFS kutokana na kuibuka kwa wananchi wanaoharibu mazingira kwa kuchimba madini na kuleta athari kubwa katika vyanzo vya maji.

Viongozi wa Jumuiya yenye Wajumbe 6 wa Kamati Kuu waliochaguliwa ni Mohamed Juma Msumari – Mwenyekiti, Amiri Salehe Ally – Makamu Mwenyekiti, Joseph Eliya Luhwago – Katibu, Tabu Ernest Sabastiano – Mhazini na Wajumbe 2 ambao ni Martha Yohana Lymo na John Peter Lukindo.