TAARIFA YA UFAFANUZI WA UTABIRI WA HALI YA MVUA KWA MWEZI JULAI KWA MWAKA 2026 KATIKA MAENEO YA BONDE LA PANGANI
TAARIFA YA UFAFANUZI WA UTABIRI WA HALI YA MVUA KWA MWEZI JULAI KWA MWAKA 2026 KATIKA MAENEO YA BONDE LA PANGANI
• WIKI YA KWANZA
Kunatarajiwa kuwa na hali ya ukavu na mvua kiasi kwa Vidakio vya Zigi, Luengera na Mkulumuzi kwa wastani wa kati ya milimita 20-50 ikijumuisha Wilaya za Mkinga, Bumbuli, Korogwe na Tanga, huku maeneo mengi ya Vidakio vya Pangani main, Kikuletwa na Umba kuwa na mvua zenye wastani wa kati ya milimita 0-20 ikijumuisha Wilaya za Pangani, Handeni, Lushoto, Kilindi, Moshi na Muheza. Halikadhalika maeneo mengine yaliyosalia yanatarajiwa kuwa makavu.
• WIKI YA PILI
Kunatarajiwa kuwa na mvua kwa maeneo yote ya Vidakio ambapo kiwango cha juu cha mvua kikitarajiwa katika Kidakio cha Mkulumuzi kwa wastani wa kati ya milimita 200-300 kwa machache katika Wilaya ya Mkinga ikifuatiwa na Kidakio cha Zigi ambacho maeneo yake mengi yakitarajiwa kuwa na mvua ya wastani wa kati ya milimita 100 – 200 haswa Wilaya ya Muheza. Maeneo mengine yaliyosalia ya Vidakio vya Msangazi, Pangani main, Mkomazi, Luengera, Kikuletwa na Umba kunatarajiwa kuwa na mvua za wastani wa kati ya milimita 20 – 50 ikijumuisha Wilaya za Pangani, Korogwe, Same, Mwanga, Mkinga, Handeni, Arumeru na Moshi. Hata hivyo, Vidakio vya Ruvu na maeneo machache ya Kidakio cha Kikuletwa, Pangani main na Umba kunatarajiwa kuwa na mvua wastani wa milimita 1-20 ikijumuisha maeneo ya Rombo, Mererani na Msitu wa tembo.
• WIKI YA TATU
Kunatarajiwa kuwa na mvua kiasi kwa maeneo yote ya Vidakio ambapo kiwango cha juu cha mvua kikitarajiwa kutokea katika Kidakio cha Mkulumuzi, Msangazi, Pangani main, Luengera na Zigi kwa wastani wa kati ya milimita 20-100 kwa maeneo machache ya Wilaya ya Mkinga, Muheza na Pangani. Maeneo mengine yaliyosalia ya Vidakio vya Umba, Kikuletwa, Ruvu na Mkomazi kunatarajiwa kuwa na wastani wa mvua wa kati ya milimita 0 – 20 ikijumuisha Wilaya za Moshi, Hai, Arumeru, Mwanga, Rombo, Same na Simanjiro.
• WIKI YA NNE
Kunatarajiwa kuwa na mvua chache zenye wastani wa kati ya milimita 0-10 kwa maeneo mengi ya Vidakio vya Pangani main, Kikuletwa, Ruvu, Luengera, Mkomazi, Zigi na Umba ikijumuisha Wilaya za Arumeru, Simanjro, Handeni, Kilindi, Korogwe, Same, Rombo na Mwanga. Maeneo mengine yanatarajiwa kuwa na hali ya ukavu kwa ujumla.

