Maadhimisho ya Bodi ya Maji Bonde la Pangani
Bodi ya Maji Bonde la Pangani inasimamia eneo bonde lenye ukubwa wa takribani kilomita za mraba 54,600 ambayo ni asilimia 93% ya Bonde zima na asilimia 7% iko Nchini Kenya inayolifanya Bonde letu kuwa ni la kimataifa (Bonde Shirikishi). Pia linalohusisha Mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Tanga na Manyara (Wilaya za Simanjiro na Kiteto) katika Halmashauri za Wilaya takribani 24. Bonde la Pangani lilianzishwa mnamo Julai 1, Mwaka 1991 na mwaka huu tarehe 1 Julai 2026 linatimiza miaka 35 tangu kuanzishwa kwake. Ili kuazimisha miaka 35 tangu kuanzishwa kwa Bonde la Pangani, Bodi imeandaa program mbalimbali ambazo zitaanza tarehe 25 Juni, 2026 na programu hizi zitakuwa kwa wiki nzima ambapo hitimisho lake litakuwa ni tarehe 1 Julai 2026.

