MATARAJIO YA HALI YA MTIRIRIKO WA MAJI KATIKA BONDE LA PANGANI KWA KUZINGATIA TAKWIMU KUTOKA TMA, OKTOBA 2026
MATARAJIO YA HALI YA MTIRIRIKO WA MAJI KATIKA BONDE LA PANGANI KWA KUZINGATIA TAKWIMU KUTOKA TMA, OKTOBA 2026
WIKI YA I- Vidakio vya Kikuletwa na Ruvu (Wilaya ya Arumeru na Rombo) kupata mvua za Wastani wa mm 20-50 hivyo kuongeza kidogo mitiririko ya maji katika mito ya Kikafu, Karanga, Weruweru,Usa, Nduruma na Themi) na kuongeza mtiririko katika Mito Mikubwa ya Kikuletwa na Ruvu hadi Bwawa la Nyumba ya Mungu.
Vidakio vya Pangani Main, Zigi, Mkulumuzi, Luengera, Msangazi, Umba na Mkomazi (Wilaya za Simanjiro, Kiteto, Same, Kilindi,Handeni,Bumbuli,Tanga, Korogwe, Lushoto, Mkinga na Muheza) kuwa na mvua wastani wa 0-20mm na kuchangia ongezeko wa mtiririko Mto Pangani.
WIKI YA II-Kidakio cha Kikuletwa na Ruvu kuwa na wastani wa Mm 20-50 na kuongeza maji katika mito ya mkoa Kilimanajro na Arusha kunatarajiwa kuwa na hali ya mvua, wastani wa Milimita 20-50 na kupelekea ongezeko la mtiririko ya maji katika mito iliyopo Mikoa ya Kilimanjaro na Arusha kuelekea Bwawa la Nyumba. Maeneo machache ya ukanda wa Pwani katika Vidakio vya Zigi, Msangazi na Mkulumuzi kuwa na mvua za wastani wa Milimita 5-10 hivyo kupelekea ongezeko la maji katika mto Zigi, Mkulumuzi, na Msangazi. Maeneo machache yaliyosalia ya Vidakio vya Pangani Main na Umba yakiendelea kupata mvua nyepesi, wastani wa Milimita 1-5 na kupelekea ongezeko dogo la mtiririko wa maji katika mto Umba na Pangani.
WIKI YA III-Kidakio cha Kikuletwa na Ruvu kwa maeneo machache kunatarajiwa kuwa na hali ya mvua za juu, wastani wa Milimita 100-300 katika Wilaya za Siha, Moshi, Hai na Rombo, hali inayotarajiwa ongezeko kubwa katika mitiririko ya maji katika mito ya Kikafu,Weruweru,Karanga, Rau, Kikuletwa, Nduruma,Themi, na Usa (Mkoa Kilimanjaro na Arusha). Halikadhalika, ukanda wa Pwani katika Vidakio vya Pangani Main, Mkulumuzi, Zigi,Umba, Luengera na Msangazi kuwa na mvua kiasi kwa wastani wa kati ya Mm 0-50 (Wilaya ya Tanga, Muheza, Kilindi, Same, Simanjiro, Kiteto, na hivyo kupelekea ongezeko la maji katika mito ya Zigi, Mkulumuzi, Luengera, Umba,Muzi, Kihuhwi na Msangazi na kuongeza ongezekoa usawa wa maji katika Bwawa la Mabayani.
WIKI YA 1V-Vidakio vya Kikuletwa na Ruvu kuwa na hali ya mvua, wastani wa Milimita 50-200 katika maeneo machache (Wilaya za Siha, Moshi na Rombo) hivyo kuchangia ongezeko la mtiririko wa Maji katika mito yote ya Mkoa Kilimanjaro na Arusha (Karanga, Kikafu, Weruweru,Himo,Rau,Mue, Usa, Kikuletwa na Sanya) hadi Bwawa la Nyumba ya Mungu. Maeneo ya Vidakio vya Msangazi, Pangani main, Mkulumuzi, Zigi, na Luengera yakitarajiwa mvua wastani wa Milimita 0-50 (Wilaya za Handeni,Tanga,Muheza na Bumbuli) na kupelekea ongezeko la maji katika Mto Pangani, Mkulumuzi, Msangazi, Muzi,na Zigi-Mkoa Tanga

