UTABIRI WA HALI YA M...
UTABIRI WA HALI YA MVUA KATIKA BONDE LA PANGANI MWEZI - NOVEMBA 2026.
05 Nov, 2026
UTABIRI WA HALI YA MVUA KATIKA BONDE LA PANGANI MWEZI - NOVEMBA 2026.

MATARAJIO YA HALI YA MTIRIRIKO WA MAJI KATIKA VYANZO VYA MAJI KATIKA BONDE LA PANGANI KWA MWEZI NOVEMBA - 2026

WIKI YA I - Vidakio vya Ruvu, Kikuletwa na Luengera kuwa na hali ya mvua zenve wastani wa Milimita 50-300 kwa maeneo machache ya Wilaya (Meru Arusha, Rombo, Hai, Moshi na Bumbuli) na kupelekea ongezeko la mtiririko wa maji katika mito ya Kikuletwa, Ruvu,na Luengera. Vidakio vya Zigi, Umba, Mkulumuzi, Pangani Main, na Msangazi Wilaya (Simanjiro, Kiteto, Same, Mwanga, Handeni, Muheza, Pangani, Kilindi, Lushoto na Mkinga) kuwa na mvua wastani wa Milimita 0-50 na kupelekea ongezeke dogo la mtiririko wa maji katika mto Mkulumuzi, Zigi, Pangani, Msangazi, na Umba.
WIKI YA II - Kidakio cha Kikuletwa, Ruvu na Mkomazi kunatarajiwa kuwa na mvua wastani wa Milimita 50-300 Wilaya (Arusha, Siha, Rombo, Same na Lushoto) na kupelekea ongezeko la mitiririko wa maii katika mto Kikuletwa, Ruvu, na Mkomazi. Vidakio vya Pangani Main, Umba, Zigi, Mkulumuzi, Msangazi na Luengera Wilaya (Simanjiro, Kiteto, Handeni, Korogwe, Muheza, Kilindi, Mkinga, Pangani na Tanga) kuwa na Mvua nyepesi wastani wa Milimita 0-50).
WIKI YA III - Vidakio vya Kikuletwa na Ruvu kuwa na mvua wastani wa Milimita 20-200, Wilaya (Arumeru, Rombo na Siha) na kupelekea ongezeko la mtirirko wa maji katika mto Kikuletwa, na Ruvu hadi Bwawa la Nyumba ya Mungu. Maeneo yaliyosalia ya Kidakio cha Pangani main, Msangazi,Mkulumuzi,Luengera,Umba, Zigi na Mkomazi kupata Mvua wastani wa Milimita 0-20 Wilaya ( Simanjiro, Kiteto, Same, Mwanga, Lushoto, Bumbuli, Handeni, Mkinga, Muheza, Kilindi, Korogwe na Tanga), na kupelekea ongezeko dogo la maji katika mto Mkulumuzi, Msangazi,Zigi na Mkomazi.
WIKI YA IV- Vidakio vya Kikuletwa, Ruvu, na Mkomazi kunatarajiwa kupata mvua wastani wa Milimita 100-300 Wilaya ( Arumeru, Siha, Moshi na Rombo). Vidakio vilivyosalia vya Umba, Mkulumuzi, Zigi, Pangani Main, Luengera na Msangazi kuwa na mvua wastani Milimita 0-100-Wilaya ya (Simanjiro, Kiteto, Mwanga, Same, Muheza, Pangani, Bumbuli, Korogwe, Handeni, Mkinga, na Tanga). Ongezekeko la mtiririko wa maji linatarajiwa katika mto Kikuletwa, Ruvu,Zigi, Mkulumuzi Msangazi na Umba,

"UTUNZAJI WA VYANZO VYA MAJI NI JUKUMU LETU SOTE "

slot gacor