MWELEKEO WA MSIMU WA...
MWELEKEO WA MSIMU WA MVUA MWEZI (MACHI - MEI, 2025) BONDE LA PANGANI.
27 Feb, 2025
MWELEKEO WA MSIMU WA MVUA MWEZI (MACHI - MEI, 2025) BONDE LA PANGANI.

Angalizo 1: Wastani wa muda mrefu wa miaka 30 (1991-2020) wa mvua za Msimu (Machi hadi Mei), mabadiliko ya mvua mwaka mmoja na mwingine yamezingatiwa.

Dondoo muhimu

  1. Mvua zinatarajiwa kuwa za wastani hadi juu ya wastani katika maeneo ya mabonde madogo (Kikuletwa, Mkomazi na Pangani_Main) na wastani hadi chini ya wastani katika maeneo ya mabonde madogo (Umba, Luengera, Zigi, Mkulumuzi na Msangazi) yaliyopo katika Bonde la Pangani.
  2. Mvua zinatarajia kuanza wiki ya wiki ya pili ya mwezi Machi, 2025.
  3. Mvua zinatarajiwa kuisha wiki ya tatu na ya nne ya mwezi Mei, 2025.

Angalizo 2

  Izingatiwe kuwa matukio ya vipindi vya mvua kubwa yanaweza kujitokeza katika msimu huu wa masika, 2025 kwenye maeneo yanayotarajiwa kupata mvua za wastani hadi juu ya wastani na matukio ya hali mbaya ya hewa ikiwemo vipindi vya mvua kubwa yanaweza kujitokeza katika maeneo yanayotarajiwa kupata mvua za wastani hadi ya wastani.

Matokeo na ushauri kwa sekta ya rasilimali maji.

Matokeo

  1. Kuathiri hali ya unyevunyevu wa udongo katika maeneo mengi ya Bonde la Pangani kwa maeneo yatakayopata mvua za watani hadi chini ya wastani hivyo kupelekea hali ya ukavu kwenye Bonde la  Pangani na kuathiri upatikanaji wa maji.
  2. Kuathiri vyanzo vya maji na mtiririko wake.
  3. Kuathirika kwa shughuli mbalimbali zinazotegemea rasilimali maji (Katika kina fulani mfano uzalishaji umeme, matumizi ya nyumbani, umwagiliaji, matumizi ya viwandani, kwa ajili ya bioanuai n.k)
  4. Kina cha maji katika Bonde la Pangani kinatarajiwa kupungua kwenye maeneo yatakayopata mvua za wastani hadi chini ya wastani na kuongezeka kwenye maeneo yatakayopata mvua za juu ya wastani.

Ushauri

  1. Kuongeza uwezo wa uvunaji   maji ya mvua kwa kujenga mabwawa na mifumo ya kuhifadhi maji kwa kipindi cha ukavu.
  2. Kutengeneza mipango ya dharura ya usambazaji na msaada kwa wakulima kwenye maeneo yanayoyotarajiwa kupata mvua za wastani hadi chini ya wastani.
  3. Bonde la Pangani na Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) inashauri Mamlaka za Maji  kushirikiana na jamii katika uhifadhi wa maji kwa matumizi endelevu.