UTABIRI WA HALI YA H...
UTABIRI WA HALI YA HEWA KATIKA BONDE LA PANGANI - FEBRUARI 2026
10 Feb, 2026
UTABIRI WA HALI YA HEWA KATIKA BONDE LA PANGANI - FEBRUARI 2026

TAARIFA YA UFAFANUZI WA UTABIRI WA HALI YA MVUA KWA MWEZI FEBRUARI 2026 KATIKA MAENEO YA BONDE LA PANGANI

•    WIKI YA KWANZA  
Katika Vidakio vya Bonde la Pangani kwa maeneo machache haswa Vidakio vya Ruvu, Umba na Kikuletwa, kunatarajiwa kuwa na hali ya ukavu. Halikadhalika baadhi ya maeneo ya Kidakio cha Mkomazi, Luengera na Msangazi yatarajiwa kuwa na mvua nyepesi zenye wastani wa chini ya Milimita Kumi (10) kwa maeneo mengi, hii ikijumuisha Wilaya za Korogwe, Handeni na Same. Mvua kubwa zimeweza kutabiriwa katika Kidakio cha Pangani Main haswa katika maeneo mengi ya Wilaya ya Simanjiro kwa kuwepo na wastani unaokadiriwa kati ya milimita 1 mpaka 100.
•    WIKI YA PILI  
Kidakio cha Pangani Main haswa Wilaya ya Simanjiro, Msangazi ikijumuisha maeneo ya Wilaya ya Handeni, Kikuletwa, Luengera na Mkomazi kuna matarajio ya kupata mvua zenye wastani wa milimita kati ya 5 – 50 kwa maeneo mengi huku maeneo mengine ya Vidakio yaliyosalia yakitarajiwa kuwa na hali ya ukavu kiasi.
•    WIKI YA TATU 
Vidakio vya Bonde la Pangani kunatarajiwa kuwa na hali ya mvua zenye wastani wa milimita 1-10 kwa mengi. Halikadhalika baadhi ya maeneo ya Kidakio cha Luengera Wilaya ya Korogwe na Kidakio cha Msangazi wilaya za Handeni, Kidakio cha Pangani main haswa Wilaya ya Simanjiro yatarajiwa kuwa na mvua za wastani wa milimita 20-50 kwa maeneo mengi huku maeneo machache yaliyosalia yakiendelea kubaki makavu kwa ujumla.
•    WIKI YA NNE 
Kwa wiki hii maeneo mengi ya Vidakio vilivyopo ndani ya Bonde la Pangani kuna matarajio ya kuwa na hali ya ukavu na mvua chache zenye wastani wa kiasi cha milimita 1-5 kwa ukanda wa mashariki mwa Bonde haswa katika maeneo mengi ya Mkoa wa Tanga katika Vidakio vya Mkulumuzi, Zigi, Luengera, Umba na Msangazi.