UTABIRI WA HALI YA M...
UTABIRI WA HALI YA MVUA KATIKA BONDE LA PANGANI MWEZI SEPTEMBA 2026.
07 Sep, 2026
UTABIRI WA HALI YA MVUA KATIKA BONDE LA PANGANI MWEZI SEPTEMBA 2026.

UTABIRI WA HALI YA MVUA BONDE LA PANGANI-SEPTEMBA, 2026

WIKI YA KWANZA - Kunatarajiwa kuwa na mvua kiasi kwa maeneo mengi kwa wastani wa kati ya Milimita 0-20 hivyo kuwa na ongezeko la mitiririko ya maji mtoni haswa mito ya Zigi, Mkulumuzi, Msangazi na Pangani katika Wilaya za Same,Korogwe, Handeni, Simanjiro na Pangani. Kidakio cha Kikuletwa na Ruvu kunatarajiwa kuwa na mvua za wastani wa kati ya Milimita 10-50 na kupelekea kuongezeka mitiririko ya maji katika mito ya Karanga, Kikafu, Weruweru na Kikuletwa. Maeneo yaliyosalia yataendelea kuwa makavu haswa Kidakio cha Mkomazi na Umba (Wilaya za Same na Lushoto). 

WIKI YA PILI - Kidakio cha Kikuletwa na Ruvu kwa maeneo machache kunatarajiwa kuwa na hali ya mvua yenye wastani wa kati ya Milimita 1-100 hivyo kuongeza mtiririko ya maji katika mito iliyopo Mikoa ya Kilimanjaro na Arusha kuelekea Bwawa la Nyumba ya Mungu kupitia mto Kikuletwa. Halikadhalika maeneo machache ya ukanda wa Pwani vidakio vya Mkulumuzi, Zigi, Luengera na Msangazi kunatarajiwa kuwa na mvua za kiasi kwa wastani wa kati ya milimita 1- 50 na kupelekea ongezeko la maji katika mito Zigi, Mkulumuzi, Luengera na Msangazi. Maeneo machache yaliyosalia yataendelea kuwa na ukavu haswa katika Kidakio cha Umba na Mkomazi (Wilaya za Same na Lushoto).

WIKI YA TATU - Kidakio cha Kikuletwa na Ruvu kwa maeneo machache kunatarajiwa kuwa na hali ya mvua za juu ya wastani kati ya Milimita 20-300 na kuongeza mitiririko ya maji mtoni katika mito ya Kikafu,Weruweru,Karanga, Rau na Kikuletwa (Mikoa ya Kilimanjaro na Arusha) kuelekea Bwawa la Nyumba ya Mungu. Halikadhalika maeneo machache ya ukanda wa Pwani (Vidakio vya Mkulumuzi, Zigi, Luengera na Msangazi) kunatarajiwa mvua za wastani wa kati ya Milimita 5-20 na kuongeza maji mito ya Zigi, Mkulumuzi, Luengera na Msangazi. Maeneo machache yaliyosalia yataendelea kuwa na mvua za chini ya milimita 5 na ukavu kiasi katika Kidakio cha Pangani, Mkomazi na Umba (Wilaya za Same, Korogwe, Simanjiro na Lushoto). 

WIKI YA NNE - Kidakio cha Kikuletwa na Ruvu kwa maeneo machache kunatarajiwa kuwa na mvua za juu ya wastani wa kati ya Milimita 20-300 kupelekea ongezeko kubwa la maji katika mitiririko ya mto Kikafu, Weruweru, Karanga, Rau na Kikuletwa (Mkoa wa Kilimanjaro na Arusha) kuelekea Bwawa la Nyumba ya Mungu. Halikadhalika maeneo ya Vidakio yaliyosalia yanatarajiwa kuwa na hali ya mvua za wastani wa kati ya Milimita 1-10 huku maeneo mengine yakiendelea kuwa makavu kwa ujumla.

"UTUNZAJI WA VYANZO VYA MAJI NI JUKUMU LETU SOTE"

slot gacor