TAARIFA YA UFAFANUZI WA UTABIRI WA HALI YA MVUA KWA WIKI MBILI ZIJAZO (MWEZI APRILI MWAKA 2026) KATIKA MAENEO YA BONDE LA PANGANI
TAARIFA YA UFAFANUZI WA UTABIRI WA HALI YA MVUA KWA WIKI MBILI ZIJAZO (MWEZI APRILI MWAKA 2026) KATIKA MAENEO YA BONDE LA PANGANI
• WIKI YA TATU
Kwa wiki hii katika Vidakio vya Pangani main, Msangazi, Kikuletwa na Ruvu kunatarajiwa kuwa na mvua zenye wastani wa milimita 0-20 kwa maeneo mengi ikijumuisha Wilaya ya Simanjiro, Same, Arumeru, Handeni, Korogwe na Lushoto. Hata hivyo kiwango cha juu cha mvua yenye wastani wa milimita kati ya 50 -300 kwa maeneo machache ikijumuisha Wilaya ya Muheza na Mkinga.
• WIKI YA NNE
Kwa wiki hii maeneo mengi ya vidakio vya Pangani main kunatarajiwa kuwa na mvua zenye wastani wa milimita 0-20 kwa maeneo mengi ikijumuisha Wilaya ya Simanjiro, Same,Handeni na Korogwe. Halikadhalika, Vidakio vilivyosalia ikiwemo Msangazi, Umba na Luengera inayojumuisha maeneo ya Wilaya ya Handeni, Muheza na Mkinga. Mvua za wastani wa kati ya milimita 50 – 200 inatarajiwa kunyesha katika maeneo ya kidakio cha Zigi ikijumuisha Wilaya ya Muheza na Mkinga.

