DC Same asimamia uta...
DC Same asimamia utatuzi wa mgogoro kati ya RUWASA na Kijiji cha Kijomu
23 Feb, 2023
DC Same asimamia utatuzi wa mgogoro kati ya RUWASA na Kijiji cha Kijomu

Bodi ya Maji Bonde la Pangani imeshiriki kikao cha pamoja kwa ajili ya kupata ufumbuzi wa mgogoro wa matumizi ya maji kati ya Wakala wa Maji vijijini Wilaya ya Same (RUWASA) na watumiaji wa Kijiji cha Kijomu kilichopo Kata ya Hedaru Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro. Kikao hicho kilichoongozwa na Mhe. Mkuu wa Wilaya ya Same Bi. Kaslida J. Mgeni kilihudhuriwa na Mkurugenzi wa Bonde la Pangani Bw. Segule A. Segule, Katibu Tawala Wilaya ya Same Ndg. Sospeter M. Magonera, Kaimu Meneja wa RUWASA Wilaya Mha. Abdallah A. Gendaeka pamoja na watumishi wa Bodi ya Maji Bonde la Pangani. Kikao hicho ni miongoni mwa mfululizo wa vikao mbalimbali ambavyo pia vimeshirikisha viongozi wa kijiji cha Kijomu ili kupata ufumbuzi wa changamoto hiyo. Bodi ya Maji Bonde la Pangani imeendelea kushirikisha viongozi mbalimbali pamoja na wadau ili kupata suluhu ya changamoto ya upatikanaji wa huduma ya maji kwa matumizi mbalimbali hususani katika kipindi cha kiangazi jambo ambalo linafanikisha kuepusha kuibuka kwa migogoro ya matumizi ya maji.

Mhe. Mkuu wa Wilaya ya Same Bi. Kaslida J. Mgeni

Bw. Segule A. Segule-Mkurugenzi wa Bonde la Pangani

Mha. Abdallah A. Gendaeka-Kaimu Meneja wa RUWASA Wilaya

Kikao cha utatuzi wa mgogoro kikiendelea

Picha ya pamoja ya wajumbe wa kikao cha usuluhishi wa mgogoro

"UTUNZAJI WA VYANZO VYA MAJI NI JUKUMU LETU SOTE"