Kampeni ya Upandaji...
Kampeni ya Upandaji Miti Bwawa la Kweng'ombe
20 May, 2023
Kampeni ya Upandaji Miti Bwawa la Kweng'ombe

Bodi ya Maji bonde la Pangani imeendesha kampeni ya upandaji miti elfu moja katika Bwawa la Kweng'ombe, Handeni Mkoani Tanga kwa lengo la kurudisha uoto wa asili katika Bwawa hilo.

Mgeni rasmi katika kampeni hiyo ambayo imefanyika tarehe 11 Mei, 2023 alikuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mhe. Albert Msando ambae ameipongeza Bodi ya Maji Bonde la Pangani kwa kuhifadhi mita 60 za Bwawa hilo. Aidha Mhe. Msando ametumia nafasi hiyo kuwaagiza Viongozi wa Halmashauri, Kata na Vijiji Kutumia Sheria ndogondogo kuhifadhi mita zaidi ya 60 kwa kuainisha shughuli zinazoweza kufanyika ili kuepuka Uchafuzi na uharibifu wa bwawa hilo.

Bodi ya Maji Bonde la Pangani ilishachukua hatua za awali za kuhifadhi Bwawa hilo kwa kuweka alama za Mipaka 55 pamoja na mabango ya makatazo ya shughuli za kibinadamu.

"Utunzaji wa Vyanzo vya Maji ji Jukumu letu sote."