MWELEKEO WA MVUA KAT...
MWELEKEO WA MVUA KATIKA ENEO LA BONDE LA PANGANI KWA KIPINDI CHA MWEZI AGOSTI 2025
07 Aug, 2025
MWELEKEO WA MVUA KATIKA ENEO LA BONDE LA PANGANI KWA KIPINDI CHA MWEZI AGOSTI 2025

MWELEKEO WA MVUA KATIKA ENEO LA BONDE LA PANGANI KWA KIPINDI CHA MWEZI AGOSTI 2025

1. UTANGULIZI

Taarifa hii inatoa mwelekeo wa mvua katika Eneo-Bonde la Pangani kwa kipindi cha mwezi Agosti 2025.

Kwa kawaida, maeneo ya Bonde la Pangani yanatarajiwa kuwa na hali ya joto kiasi na baridi la wastani katika kipindi cha mwezi Agosti 2025 yakiambatana na vipindi virefu vya ukavu katika baadhi ya maeneo.

2. MWELEKEO WA MVUA KATIKA ENEO LA BONDE LA PANGANI KWA KIPINDI CHA MWEZI AGOSTI 2025

Katika kipindi cha mwezi Agosti 2025, hali ya ukavu kwa ujumla inatarajiwa katika maeneo ya Bonde la Pangani isipokuwa upande wa Mashariki, ambapo mvua nyepesi katika maeneo machache zinatarajiwa.

Utabiri wa mtawanyiko wa mvua kwa kila wiki, umetolewa kwa ushirikiano baina ya Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) na Bodi ya Maji Bonde la Pangani (PBWB).

  •         WIKI YA KWANZA 

Kwa wiki hii, katika maeneo ya Vidakio (Catchments) vya Bonde la Pangani kunatarajiwa kuwa na hali ya ukavu kwa ujumla. Halikadhalika baadhi ya maeneo ya Kidakio cha Mkomazi na Msangazi yatarajiwa kuwa na mvua nyepesi zenye wastani wa chini ya Milimita Kumi (10mm) kwa maeneo machache.

•            WIKI YA PILI 

Kwa wiki hii, katika Kidakio cha Mto Umba, Zigi, Ruvu, Msangazi na Kikuletwa kuna matarajio ya kupata wastani wa mvua chini ya Milimita Kumi (10mm) huku Kidakio cha Pangani Mainstem na Msangazi kukitarajiwa kuwa na hali ya ukavu haswa katika Wilaya za Same kwa Mkoa wa Kilimanjaro na Korogwe kwa Mkoa wa Tanga.

•            WIKI YA TATU

Kwa wiki hii, katika vidakio vya Bonde la Pangani kunatarajiwa kuwa na hali ya ukavu kwa ujumla. Halikadhalika baadhi ya maeneo ya Kidakio cha Luengera Wilaya ya Korogwe na Kidakio cha Msangazi Wilaya Handeni yatarajiwa kuwa na mvua nyepesi zenye wastani wa chini ya Milimita Kumi (10mm) kwa maeneo machache.

•             WIKI YA NNE

Kwa wiki hii, kuna matarajio ya kupata mvua chache za wastani wa Milimita Tano hadi Hamsini (5mm-50mm) kwa ukanda wa mashariki mwa Bonde haswa katika maeneo mengi ya Mkoa wa Tanga katika Vidakio vya Mkulumuzi Wilaya Muheza, Pangani na Tanga; Kidakio cha Zigi katika Wilaya Muheza na Mkinga; Kidakio cha Luengera katika Wilaya Korogwe na Muheza; Kidakio cha Umba katika Wilaya Lushoto na Mkinga; na Kidakio cha Msangazi katika Wilaya Handeni. Hata, hivyo maeneo yaliyosalia yanatarajiwa kuwa na mvua chache na hali ya ukavu kwa ujumla.