TAARIFA YA UFAFANUZI WA UTABIRI WA HALI YA MVUA KWA MWEZI JANUARI KWA MWAKA 2025 KATIKA MAENEO YA BONDE LA PANGANI
TAARIFA YA UFAFANUZI WA UTABIRI WA HALI YA MVUA KWA MWEZI JANUARI KWA MWAKA 2025 KATIKA MAENEO YA BONDE LA PANGANI
• WIKI YA KWANZA
Kwa wiki hii, Kidakio cha Mkomazi katika baadhi ya maeneo ya Wilaya Same, Kidakio cha Msangazi Wilaya Handeni, Kilindi na Korogwe; Kidakio cha Luengera baadhi ya maeneo ya Vijiji na Kata za Wilaya Korogwe na Lushoto; Kidakio cha Zigi baadhi ya maeneo ya Kata na Vijiji vya Wilaya Muheza, Korogwe na Tanga; Kidakio cha Kikuletwa baadhi ya maeneo ya Kata na Vijiji vya Wilaya Arumeru, Siha, Hai, Simanjiro na Moshi pamoja na baadhi ya maeneo machache ya Kidakio cha Pangani Mainstem Wilaya Mwanga, Same, Simanjiro, Korogwe, Muheza na Pangani yakitabiriwa kuwa na kiasi cha mvua ya wastani usiozidi Milimita 20 huku upande wa Kidakio cha Pangani Mainstem kwenye baadhi ya maeneo ya Wilaya Same, Mwanga, Korogwe na Pangani ikitabiliwa kuwa na mvua kiasi kwa wastani wa milimita 50. Halikadhalika baadhi ya maeneo ya Kidakio cha Umba-Wilaya Lushoto na Kidakio cha Ruvu baadhi ya maeneo Wilaya Rombo, Mwanga na Moshi yakisalia kuwa makavu kiasi.
• WIKI YA PILI
Kwa wiki hii baadhi ya maeneo katika kidakio cha Umba Wilaya Lushoto; Kidakio cha Mkomazi Wilaya Same; Kidakio cha Zigi Wilaya Muheza, Korogwe, Mkinga na Tanga, Kidakio cha Ruvu, Pangani na Kikuletwa kuna matarajio ya kupata mvua za wastani chini ya milimita 20 huku ukanda wa kusini mwa Kidakio cha Pangani Mainstem na Msangazi Wilaya Handeni na Kilindi yakitarajiwa kuwa na mvua zenye wastani mkubwa kiasi usiozidi milimita 200. Halikadhalika baadhi ya maeneo ya Kidakio cha Kikuletwa na Ruvu yakisalia kuwa makavu kiasi.
• WIKI YA TATU
Kwa wiki hii baadhi ya maeneo katika Kidakio cha Mkulumuzi Wilaya Muheza na Tanga; Kidakio cha Zigi Wilaya Korogwe, Muheza, Mkinga na Tanga; Kidakio cha Mkomazi Wilaya Same na Korogwe na Lushoto; Kidakio cha Luengera Wilaya Korogwe na Lushoto; Kidakio cha Ruvu Wilaya Moshi, Mwanga na Rombo na Kidakio cha Umba Wilaya Lushoto matarajio ya kupata mvua chache za wastani wa chini ya milimita 10 huku maeneo mengi ya Kidakio cha Pangani Mainstem na Kikuletwa yakitabiriwa kuwa na mvua za kiasi kisichozidi wastani wa milimita 20 na baadhi ya maeneo ya Wilaya ya Simanjiro kupata mvua za wastani wa milimita zisizozidi 50.
• WIKI YA NNE
Kwa wiki hii baadhi ya maeneo katika Kidakio cha Mkulumuzi; Ruvu na Umba kuna matarajio ya kupata mvua chache za wastani wa chini ya milimita 10 huku maeneo mengi ya vidakio vya Pangani Mainstem, Msangazi, Zigi, Mkomazi na Kikuletwa yakitabiriwa kuwa na mvua za wastani kiasi kisichozidi milimita 100 .