Ujenzi wa Bwawa la H...
Ujenzi wa Bwawa la Horohoro Kunufaisha Wananchi 26,000
02 Oct, 2023
Ujenzi wa Bwawa la Horohoro Kunufaisha Wananchi 26,000

Bodi ya Maji Bonde la Pangani inatekeleza Mradi wa ujenzi wa Bwawa la Horohoro lililoko katika Kijiji cha Horohoro Boda Kata ya Duga, Wilaya ya Mkinga, Mkoa wa Tanga ambao umeendelea mnamo tarehe 9 Agosti, 2023 baada ya kusitishwa ili kupisha kipindi cha mvua. Mpaka sasa ujenzi wa Bwawa umefikia asilimia 85% na unatarajia kukamilika ifikapo tarehe 15 Oktoba, 2023. Mara litakapokamilika, Bwawa hili linakadiriwa kuhifadhi lita Milioni 70.4 na litanufaisha wananchi takribani 26,000 waishio katika Mji wa Horohoro na vijiji vya jirani. Aidha Bwawa hili ndilo chanzo pekee cha uhakika cha Maji kinachoenda kutatua changamoto ya Maji katika Mji wa Horohoro kutokana na kutokuwepo kwa mito yenye maji ya kutosha wala maji chini ya ardhi.

“UTUNZAJI WA VYANZO VYA MAJI NI JUKUMU LETU SOTE”