Maadhimisho ya Siku...
Maadhimisho ya Siku ya Pangani
19 Jun, 2022 08:00AM - 04:00PM Tanga, Arusha, Kilimanjaro & Manyara
Maadhimisho ya Siku ya Pangani
Usimamizi wa Rasilimali za Maji una historia ndefu kuanzia miaka 46 iliyopita ambao umepitia mabadiliko mbalimbali ya Kisera na Kisheria. Mabadiliko hayo yamepelekea kuundwa kwa Bodi tisa za mabonde nchini kwa upande wa Tanzania bara ambapo Bonde la Pangani ndilo lililokuwa la kwanza kuanzishwa mwaka 1991 likiwa la majaribio chini ya Sheria ya Matumizi ya Maji Na. 42 ya Mwaka 1974 kama ilivyorekebishwa na Sheria Na. 10 ya Mwaka 1981 chini ya kifungu Na. 7 (1). Sheria hiyo imefutwa kupitia kifungu Na. 22 cha Sheria ya Usimamizi wa Rasilimali za Maji Na. 11 ya Mwaka 2009. Malengo makuu ya Bodi za Maji za Mabonde ni pamoja na kutekeleza dhana ya Usimamizi Shirikishi na Endelevu wa Rasilimali za Maji kwa ajili ya kuimarisha shughuli za kijamii na kiuchumi.
Katika kuadhimisha siku ya kuanzishwa kwa Bonde la Pangani mnamo tareh 1,Julai, 1991 Bodi imeandaa maadhimisho ya Wiki ya Pangani yatakayofanyika kuanzia tarehe 25 Juni, 2022 hadi tarehe 01 Julai, 2022 ambapo shughuli mbalimbali zitafanyika ikiwemo Maonyesho, usafi katika vyanzo vya Maji, mkutano wa wadau na uelimishaji wa Jamii
 
Wote Mnakaribishwa