Je nawezaje kuomba k...
Je nawezaje kuomba kibali cha Matumizi ya Maji?
  1. Andika barua kwa Afisa wa Maji Bonde la Pangani kupitia kwa Mwenyekiti wa Kijiji/Mtaa unaohusika.
  • Barua itaje jina la chanzo, mahali kilipo, madhumuni ya kuomba kibali cha kutumia maji, kiasi cha maji kinachohitajika na wanufaika walioko karibu na chanzo hicho.
  • Kama eneo analotoka mwombaji wa kibali kuna Umoja wa Watumia Maji uliosajiliwa kwa mujibu wa Sheria ya Usimamizi wa rasilimali za Maji Na.11 ya Mwaka 2009, anatakiwa apitishe barua ya ombi kwa Mwenyekiti wa Umoja.

 

  1. Mwombaji atajaza fomu maalum ya maombi ya kibali cha kutumia maji na kuzirudisha kwa Mkurugenzi wa Bodi ya Maji Bonde la Pangani. Fomu hiyo italipiwa gharama za maombi ya shilingi 60,000 kwa miradi midogo ya kijamii na 250,000/= kwa miradi binafsi ya  taasisi, viwanda, mashamba makubwa, kampuni.

 

 

  1. Ofisi ya Bodi ya Maji ya Bonde:
  1. Ofisi itamwandikia mwombaji juu ya barua yake kupokelewa na kusajiliwa rasmi katika rejesta ya Bonde na kumjulisha namba ya ombi lake.
  2. Ofisi itawaandikia wadau mbalimbali kutaka maoni yao kama kutolewa kwa kibali cha kutumia maji kutaathiri miradi mingine katika eneo husika au kuleta mgogoro kwa jamii (Wadau – Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya husika, Watumiaji wakubwa katika eneo husika na Umoja wa Watumia Maji).
  3. Matangazo yatapelekwa kwa wafuatao:-
  • Ofisi za Mkuu wa Wilaya na Halmashauri ya Wilaya husika kwa ajili ya kuweka kwenye mbao za matangaazo ili kuwezesha mwenye nia ya kupinga kutolewa kwa kibali cha kutumia maji kufanya hivyo.
  • Mkurugenzi wa Rasilimali za Maji Wizara ya Maji Dar es Salaam (Kwa taarifa na kulitangaza ombi katika gazeti la serikali).
  • Katibu Tawala wa Wilaya husika.
  • Jumuiya ya watumia maji katika kidakio husika.

Muhimu: Maoni yanatakiwa kutolewa ndani ya siku arobaini (40) tangu ombi linapotangazwa.

  1. Mteja atalazimika kufanyiwa utafiti wa kihaidrolojia ili kujua uwezo wa chanzo endapo anataka kuchepusha maji kutoka kwenye chemchem, Mto au bwawa. Gharama ya utafiti wa kihadrolojia ni shilingi 1,000,000/=. Muombaji wa kibali cha kuchukua maji kwenye kisima hatalazimika kufanyiwa tathmini ya kihydrolojia isipokua atalazimika kuletwa taarifa za kisima chake kama viambatanisho vya maombi ya kibali.
  2. Ofisi itachukua taarifa ya tathmini ya mazingira (EIA) ya miradi husika kutoka kwa waombaji kwa miradi yenye uhitaji wa kufanyiwa tathmini hiyo.
  3. Ofisi itaandaa maombi yaliyokamilika ili yafikishwe katika kikao cha Bodi kwa ajili ya kutolea maamuzi.
  4. Ofisi itawaarifu waombaji kuhusu maamuzi ya kikao cha Bodi.
  5. Ofisi itaandaa vibali na kuwapa taarifa wahusika kwa ajili ya kuvichukua.

 

  1. Bodi ya Maji

1. Bodi ya Maji ya Bonde inaweza kutoa kibali cha kuchepusha, kukinga, kutunza, kuchukua na kutumia Maji kutoka chanzo cha maji kwa kutaja kiasi cha maji yatakayochukuliwa, matumizi yake na kutoa masharti kwa kipindi ambacho kitaelezwa kwenye kibali

2. Bodi ya Maji ya Bonde inaweza kutoa kibali cha muda kwa mwombaji kwa matumizi na masharti ambayo Bodi itaona yanafaa

Muhimu:

  • Kibali cha matumizi ya maji kinaweza kutolewa au kukataliwa
  • Mwombaji ana nafasi ya kukata rufaa dhidi ya Bodi
  • Kibali cha kutumia maji kinapotolewa hakimaanishi kuwa ubora na wingi wa maji ulioelezwa kwenye kibali utakuwepo
  • Kibali cha kutumia maji kinaweza kuwa ni sehemu ya haki ya kumiliki ardhi, hivyo mtu anayemiliki ardhi hiyo atakuwa na haki ya kutumia kiasi cha maji kilichoelezwa  kwenye kibali
  • Bodi ya Maji ya Bonde inaweza kupunguza kiasi cha Maji kilichoruhusiwa kwenye kibali endapo maji yaliyopo kwenye chanzo hayatoshi

 

  1. Wajibu wa watumia maji
  • Kuomba vibali vya kutumia maji kwa mujibu wa Sheria ya Usimamizi wa Rasilimali za Maji Na.11 ya Mwaka 2009
  • Kulipa ada za matumizi ya maji kwa mujibu wa Sheria ya Usimamizi wa Rasilimali za Maji Na.11 ya Mwaka 2009
  • Kuchukua kiasi cha maji kilichokubalika/kilichoruhusiwa katika kibali
  • Kurudisha maji mtoni baada ya matumizi katika hali ya usafi inayokubalika
  • Kulipa ada zilizopo kisheria
  • Kuhakikisha maji yanakuwepo kwa ajili ya mazingira kama inavyoelekezwa katika sera na sheria
  • Kuimarisha ujirani mwema ili kuepusha migogoro ya matumizi ya maji
  • Asisababishe au kuruhusu maji kuchafuliwa
  • Kuzuia uharibifu wa aina yoyote kwenye chanzo ambacho amepewa kibali
  • Kuhakikisha maji yanapita kwenye ardhi kwa usahihi na kuidhinishwa na Bodi ya Maji ya Bonde
  • Kuwasilisha kwenye Bodi ya Maji ya Bonde takwimu/taarifa sahihi za matumizi ya maji
  • Kuzingatia masharti na kanuni zilizotengenezwa kwa mujibu wa Sheria
  • Kuzingatia masharti mengine yoyote maalum yatakayoelekezwa kwenye kibali
  • Kuhakikisha kuwa maji yanatumiwa kwa ufanisi
  • Kuzingatia kifungu cha 60 cha Sheria ya Usimamizi wa Mazingira 2004 sura ya 191 ambacho kinahusu majukumu ya utoaji taarifa za athari za mazingira zitakazotokana na matumizi ya maji

 

  1. Faida ya kibali cha kutumia maji
  • Rahisi kutengeneza mizania ya maji katika chanzo chochote
  • Kujihakikishia matumizi ya maji kisheria
  • Kuwa na sauti katika matumizi ya maji
  • Kuwa na uwezo wa kukopa

Rahisi kupata ufadhili.